“Ni Vita Yetu Sote, Tukipata Viongozi Wabaya Tunaumia Wote” -Askofu Chengula

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

“Ni vita yetu sote, tukipata viongozi wabaya tunaumia wote” -Askofu Chengula
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya, Evaristo Marc Chengula, amewataka waumini wa kanisa hilo nchini Tanzania kuchagua viongozi sahihi na watakaokidhi mahitaji yao badala ya kufanya makosa kwa kuchagua viongozi wasiofaa na kuanza kulalamika baada ya uchaguzi.

Askofu Chengula ametoa ujumbe huo katika mahubiri aliyotoa kwenye ibada ya Ijumaa Kuu inayofanyika katika Kanisa la Bikira Maria wa Fatima Parokia ya Mtakifu Francisco wa Asizi, Mwanjelwa mkoani Mbeya.

Amesema imekuwa ni kawaida kwa maaskofu na wadau wengine kuanza kukosoa viongozi baada ya uchaguzi, jambo ambalo halina faida, hivyo wao kama maaskofu mwaka huu wameamua kuwataka waumini wao kuwapima kwa umakini watu wote watakaojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo.

“Ni vita yetu sote, tukipata viongozi wabaya tunaumia wote, tukipata viongozi wazuri tutafurahi wote, kila mmoja aone kiu ya Tanzania hii kuwa nchi ya upendo,” -Askofu Chengula
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa sasa hatuna viongozi wabaya bali baadhi ya raia wabaya.

    ReplyDelete

Top Post Ad