Wabunge Sita Wapata Ajari Morogoro Mmoja Hali Mbaya Awekwa ICU

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wabunge Sita Wapata Ajari Morogoro Mmoja Hali Mbaya Awekwa ICU
Wabunge sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepata ajali ya gari jana usiku Machi 29, 2018 mkoani Morogoro wakati wakitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam.

Baada ya kutokea ajali hiyo saa 2 usiku katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la Bwawani, wabunge hao waliumia maeneo mbalimbali ya miili yao na kukimbizwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Wabunge hao ambao wote ni kutoka Zanzibar ni Haji Ameir Haji (Makunduchi), Khamis Ali Vuai (Mkwajuni), Bhagwanji Maganlal Meisuria (Chwaka), Makame Mashaka Foum (Kijini), Juma Othman Hija (Tumbatu).

Mganga mfawidhi hospitali ya rufaa Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya amesema majeruhi hao walipokelewa saa 3 usiku na kupatiwa huduma za awali.

"Jana tumepokea majeruhi sita walioumia sehemu mbalimbali na mmoja wao alilazimika kulazwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu (ICU) lakini hali yake inaendelea vizuri,” amesema.

“Leo asubuhi tayari tumewapa rufaa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi  zaidi.”

Dk Rita amesema Kimbe na May ndio wameumia zaidi, kupata maumivu makali.

Taarifa zilizoifikia MCL Digital zinaeleza kuwa wabunge hao wanasafirishwa kwa ndege hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad