Cannavaro Aipa 'Salute' Simba SC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Cannavaro aipa 'salute' Simba SC
Nahodha wa Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amefunguka na kudai kuwa bado hawajakata tamaa katika kuutetea ubingwa wao japo kuwa Simba SC wamewaacha kwa kiasi kikubwa katika msimamo wa ligi mpaka sasa.


Cannavaro amebainisha hayo baada ya kikosi chake kuwasili katika ardhi ya Tanzania na muda huo huo kikiunganisha kwenda jijini Mbeya kwa lengo la kujiweka sawa kuelekea mchezo wake wa kesho dhidi ya Mbeya City ikiwa ni muendelezo wa michuano ya ligi.

"Nawaheshimu Simba SC kwa kuwa ni timu ambayo nzuri nasi pia ni wazuri ila tu kwenye ligi lolote linawezekana. Nitaendelea kuwa-control vijana waendelee kupambana mpaka jasho la mwisho kwasababu bado tuna matumaini ya kuutetea ubingwa wetu. Najua bado itakuwa kazi ni ngumu ila hatujakata tamaa kwasababu kwenye mpira lolote linawezekana likatokea", amesema Cannavaro.

Mpaka dakika hii Simba bado wanaendelea kushikilia kilele msimamo wa ligi kuu kwa alama 58, Yanga akiwa nafasi ya pili kwa alama 47 huku Azam FC ikiwa ya tatu kwa alama 46.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad