Hii Hapa Tarehe Ambayo TTF Itakayowakabizi Yanga Milion 600 za CAF

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hii Hapa Tarehe Ambayo TTF Itakayowakabizi 600 M za CAF
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeibuka na kusema kuwa Klabu ya Yanga itakabidhiwa fedha zao za kuingia hatua ya makundi ya Caf mara baada ya kumalizika hatua hiyo na si sasa kama wadau wengi wanavyodhania kuwa watapata mara baada ya kuingia katika hatua hiyo.

Yanga imefanikiwa kuingia katika hatua ya makundi mara baada ya kuiondoa Wolaitta Dicha ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 2-1, na watavuna kiasi cha shilingi milioni 600 kama wakimaliza katika nafasi ya nne.
Aidha makundi ya michuano hiyo tayari yameshatangazwa juzi Jumamosi ambapo im­epangwa Kundi D ikiwa ni pamoja na Gor Mahia ya Kenya, Rayon Sport ya Rwanda na USM Alger ya Algeria.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ephraim August, amesema kuwa, Yanga haiwezi kukabidhiwa fedha zake sasa kwa kuwa haiju­likani itamaliza nafasi ya ngapi, kwani kadiri inavyomaliza nafasi za juu, ndivyo fedha zinavyoongezeka.
“Milioni 600 ambayo inatajwa Yanga kuzipata baada ya kuingia hatua ya makundi, iwapo watamaliza mi­chuano hiyo wakiwa wa mwisho kwenye kundi lao na iwapo watapanda na kumaliza wa pili kutoka chini, watapata milioni 750 na wakipiga hatua na kumaliza wa tatu kutoka chini watapewa milioni 850.

“Bingwa ka­tika michuano ya Caf anaibuka na kitita cha shilingi bilioni 2.8, mshindi wa pili bilioni 1.2 na nusu fainali atachukua bilioni 1,” alisema.
Aliongeza: “Caf ha­wawezi kutoa fedha sasa hivi kwa kuwa hakuna anayejua timu ipi itamaliza katika nafasi ya ngapi, na vilevile hawatoi kabla kwa kuhofia timu inaweza kutoshiriki michuano.”
Khadija Mngwai, Dar es Salaam.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad