TFF Yamtanga Makonda Kuwa Mgeni Rasmi Mechi ya Simba, Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makonda Kuwangoza Mashabiki wa Simba, Yanga Jumapili Taifa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtangaza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara ambao utawakutanisha Simba na Yanga Aprili 29, 2018 katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.


Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Afisa habari wa TFF, Cliford Mario Ndimbo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema Mhe. Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu watakaojitokeza kweye uwanja huo kushuhudia mchezo huo namba 178 utakaoanza saa 10 jioni.

Aidha, Cliford amesema mpaka kufikia sasa tayari tiketi za mchezo huo zinaendelea kuuzwa ambapo VIP A ni shilingi 30,000, VIP B na C 20,000 na mzunguko (Jukwaa la rangi ya Chungwa,Kijani na Bluu) 7,000.

Simba wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 59 ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 23.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad