Watu 10 Wauawa kwa Kugongwa na Gari la Mizigo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watu 10 Wauawa kwa Kugongwa na Gari la Mizigo
Watu tisa wameuawa mjini Toronto, nchini Canada baada kugongwa na gari la mizigo ambalo lilielekea kati ka mtaa wenye watu wengi. Wengine 16 wamejeruhiwa pia.
Mashuhuda wanasema kuwa dereva huyo aliendelea kuliendesha gari takribani umbali wa kilomita moja hivi.
Diego de Matos yeye alikuwa akiendesha gari lake karibu na eneo hilo,ameiambia BBC kuwa aliona watu wawili wakigongwa na gari hilo la mizigo.
"Lori hilo liliwagonga mwanamke na mwanaume.Hata hivyo baada ya kuwagonga watu hao dereva wa gari hilo aliendelea kuendesha gari hilo ambapo,mita chache mbele kulikuwa na miili mitano ama sita ikiwa chini.Na inavyoonekana dereva alikuwa akiyumbisha gari nje mara ndani ya mtaa huo,ilikuwa ni jambo la kutisha." Diego De Matos
Waziri wa usalama wa Canada Ralph Goodale amewaambia waandishi wa habari kwamba ni mapema kusema tukio hilo ni la kigaidi.
"Kuna ushirikiano wa kutosha kwa Polisi,katika kuchunguza jambo hilo,na tutatoa majibu ya hili kwa umma.Lakini kwa sasa hakuna taarifa zozote kwangu kuhusiana na chanzo ama lengo la tukio hili.'' Ralph Goodale
Kumekuwa na matukio ya magari makubwa kutumiwa na magaidi kusababisha vifo katika maeneo yenye mikusanyiko,baada ya mamlaka za usalama kudhibiti njia za magaidi hao zilizooeleka.
Matumizi ya magari makubwa ya mizigo,ni mfumo mpya ambao umekuwa ukitumiwa na magaidi kutekeleza azma yao kufuatia kubainika kwa njia zao zilizo mara zote.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad