Kumbe Ndugu wa Masogange Hawajapewa Mchango Uliochangwa na Kamati ya Wasanii Siri Yavuja

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kumbe Ndugu wa Masogange Hawapewa Mchango Uliochangwa na Kamati ya Wasanii Siri Yavuja
Ndugu wa marehemu Masogange wakiwemo wifi zake ambao pia ndio wanaishi na mtoto wake Sania, wamesema hawajapata taarifa zozote juu ya pesa ambazo zilichangwa na kamati ya wasanii, kwa ajili ya kumsaidia mtoto.


Wakizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, mmoja wa ndugu hao aliyejulikana kwa jina la Sada, amesema hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa kamati hiyo iliyoundwa na wasanii, ambayo pia ilisimamia kwa kiasi kikubwa mazishi ya Agnes Masogange, na wala hawajawasiliana nao.

“Toka tumekuja hatujapata taarifa zozote, bado hatujawasiliana nao mpaka dakika hii, labda mpaka tuwatafute”, amesema Sania.

Sambamba na hilo ndugu hao wamesema wao wenyewe kama familia wamejipanga kumlea mtoto huyo kwani walikuwa wanamlea hata wakati wa uhai wa mama yake Agnes Masogange.

Baada ya Agness Masogange kufariki kamati maalum iliyoundwa na wasanii mbali mbali wa bongo movie na filamu, walichangisha pesa kwa ajili ya kumsaidia mtoto wa marehemu Sania, ili iweze kumsaidia atakapoingia kidato cha kwanza.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad