Polisi Yafunguka Chanzo cha Ajal Iliyowaua Maofisa Watatu wa TIC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Polisi Yafunguka Chanzo cha Ajal Iliyowaua Maofisa Watatu wa TIC
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limesema uzembe wa dereva aliyekuwa akiendesha gari aina ya LandCruiser mali ya Serikali ya Tanzania ndiyo chanzo cha ajali ya gari hilo kugongana na lori na kusababisha vifo vya watu watatu, wawili kujeruhiwa.

Ajali hiyo imetokea jana Mei 21, 2018 katika Kijiji cha Msoga Chalinze Mkoa wa Pwani.

Akizungumza leo Jumanne Mei 22, 2018 Kamanda wa Polisi mkoani humo, Jonathan Shanna amesema watakuwa wakali kwa madereva watakaokiuka sheria za usalama barabara bila kujali wadhifa wao.

Amesema dereva wa gari hilo alihamia upande mwingine wa barabara wakati anayapita magari mengine bila kutazama mbele, hivyo kuligonga lori hilo.

"Sheria za usalama barabarani hazina watu maalumu wa kuzitii, sio kwamba ukiwa dereva wa ofisa wa Serikali basi wewe uende tu hovyo au ukiwa muajiriwa wa Serikali napo ujione mwamba, hata kama ni dereva wangu tutakushughulikia tu,” amesema.

Akisimulia ajali hiyo, amesema watu watatu ambao ni watumishi wa Serikali wakiwa safarini kwenda Dodoma kikazi  walifariki dunia katika ajali hiyo.

Amewataja waliofariki dunia kuwa ni Martin Laurence (39), Zacharia Nalinga (49) na Said Moshi, miili yao  imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Kibaha.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad