TFF Yawapa Agizo Yanga la Kufanya Uchaguzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

TFF Yawapa Agizo Yanga la Kufanya Uchaguzi
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeitaka klabu ya Yanga kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi za viongozi wake waliojiuzulu ikiwemo ya Mwenyekiti kwa wakati kwani tayari muda umeshapita.


Agizo hilo limetolewa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Revocatus Kuuli  na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Herman Julius akimtaka kuhakikisha klabu ya Yanga na nyingine zinafanya uchaguzi haraka iwezekanvyo.

Mbali na Yanga klabu nyingine zinazotakiwa kufanya uchaguzi kwasasa ni  AFC ya Arusha ambayo inashiriki Ligi daraja la kwanza  na Coastal Union ya Tanga ambayo imerejea ligi kuu msimu huu.

Yanga imekuwa chini ya Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti, Yussuf Manji Mei mwaka jana ambapo imetimiza mwaka saa ikiwa bila Mwenyekiti.

Tayari klabu ya Yanga imeshatangaza kufanya mkutano mkuu wa wanachama mwezi ujao na huenda moja ya agenda katika mkutano huo zinaweza kuwa ni uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakaoipatia viongozi wapya.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad