Ghana Yavunja Chama cha soka Kutokana na Tuhuma za Rushwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ghana Yavunja Chama cha soka Kutokana na Tuhuma za Rushwa
Ghana imevunjilia mbali chama cha soka baada ya rais wake kunaswa katika video akionekana akipokea 'zawadi ya pesa'.

Kwesi Nyantakyi alipigwa picha akipokea $65,000 kutoka kwa mwandishi habari mpekuzi aliyejifanya kuwa mfanyibiashara aliye na hamu kubwa kuwekeza katika soka Ghana.

Mpaka sasa hajasema chochote kuhusu tuhuma hizo.

Waziri wa michezo Isaac Asiama amesema chama hicho 'kimevunjiliwa mbali mara moja' mtandao wa GhanaWeb umeripoti.

Waandishi wanasema uchunguzi huo uliofanywa na mwandishi habari anayekumbwa na mzozo Anas Aremayaw Anas umezusha maswali kuhusu soka barani Afrika.

Katika makala hiyo ndefu, iliopewa jina 'wakati ulafi na rushwa zinapokuwa kawaida', ilikabidhiwa kwa maafisa wa serikali mwezi uliopita na kuonyeshwa wazi mbele ya umma kwa mara ya kwanza siku ya Jumatano.

Amesema hatua za muda za kuongoza soka Ghana zitatangazwa hivi karibuni, kukisubiriwa kuundwa chama kipya.

Nyantakyi ni makamu wa rais wa shirikisho la kandanda Afrika na pia mwanachama katika baraza la Fifa - taasisi inayosimamia soka duniani.

Tangu achukuwe uongozi wa chama cha GFA, ametuma ujumbe mkuu dhidi ya kupambana na rushwa.

Hatahivyo katika makala hiyo ya upekuzi inamuonyesha akiweka pesa hizo $65,000 "za kununua vitu" katika mfuko mweusi wa plastiki.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad