Kwa Mara ya Kwanza Toka Aingie Ikulu Trump Afuturu na Waislam White House

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwa Mara ya Kwanza Toka Aingie Ikulu Trump Afuturu na Waislam White House
Rais Donald Trump wa Marekani kwa mara ya kwanza tangu kuingia ofisini alifuturu pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu katika ikulu ya White House.

Ingawa White House haijatoa orodha kamili ya wageni walioalikwa kwenye hafla hiyo, waandishi wa habari waliohudhuria wamedokeza kwamba wengi wa waliokuwepo walikuwa maafisa wa serikali na mabalozi wa nchi za Kiislamu.

Ni mara ya kwanza kwa Trump kufuturu na waislamu White House baada ya kuepuka zoezi hilo mwaka jana. Kwa miongo kadhaa imekuwa kama desturi kwa marais wa Marekani kufuturu na waislamu katika ikulu wakati wa Ramadhan.

Licha ya hatua ya Trump ya kualika waumini wa dini ya Kiislamu kufuturu kwenye ikulu, mamia ya watu walikusanyika nje ya White House kupinga rais huyo kwa sera na matamshi mabaya dhidi ya dini ya Kiislamu wakati wa kampeni na hata wakati wake kama rais.

Rais huyo pia amekemewa kwa kupitisha marufuku ya usafiri dhidi ya wasafiri wanaotoka nchi za Kiislamu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad