Makonda Kujenga Viwanja Vitano vya Michezo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makonda Kujenga Viwanja Vitano vya Michezo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amefanikiwa kupata wadau watakaojenga Viwanja 5 vya Basketball (in door) kwenye wilaya zote tano za Mkoa huo kwa lengo la kuimarisha sekta ya michezo.

Makonda amesema Viwanja hivyo pia vitaweza kutumika kwa Michezo zaidi ya Mitano ikiwemo Ngumi, Mieleka, Volleyball na Table Tennis ambapo kila kiwanja kitakuwa na uwezo wa kupokea Mashabiki 3,000.

Aidha  Makonda amemchagua Mchezaji maarufu wa Basketball Bwana Hasheem Thabit kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa viwanja hivyo ambapo ujenzi wa kiwanja kimoja peke inakadiriwa kugharimu Kati ya Shilling Million 300 hadi 500.



Uamuzi wa Makonda kuja na mkakati wa kujenga Viwanja hivyo ni baada ya kubaini uwepo wa idadi kubwa ya vijana wanaopenda michezo kwenye mkoa wake lakini wanashindwa kufanyia kazi vipaji vyao kutokana na changamoto za ubovu wa miundombinu ya viwanja vya michezo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad