Mess Amponza Mama Yake Kisa Hiki Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mess Amponza Mama Yake Kisa Hiki Hapa
Wakati timu ya taifa ya Argentina ikitarajiwa kutua dimbani leo katika mchezo wake dhidi ya Croatia, mama wa Nyota wa timu hiyo Lionel Messi amesema kuwa anasikitishwa na kitendo cha mwanae kushambuliwa kwa maneno na mashabiki kwa tukio la kukosa penati.

Celia Cucittini ambaye ni mama mzazi wa Messi amesema kuwa kinachoendelea kwa sasa kuhusu mwane na kueleza kusikitishwa na hali hiyo huku akisema Messi anaumia sana kwa hali hii ya sasa na wamuache kwa kuwa analipambania taifa.

“tangu Messi akose penati kumekuwa na maneno mengi mabaya juu yake na mashabiki wa timu ya taifa ya Argentina pia wamekuwa wakimshambulia sana kwa maneno, kama kuna mtu anataka kurudi na kombe nyumbani basi Messi namba moja”, amesema mzazi huyo.

Kubwa tangu michuano ya kombe la dunia ianze ni tukio la nyota wa Argentina Lionel Messi kukosa tuta katika mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya timu ya taifa ya Iceland.

Hadi sasa Argentina wana alama moja tu katika kundi lao D na hii leo watakipiga dhidi ya Croatia huku Gabriel Mercado akionya kwamba Messi ana njaa kali ya kumwadhibu yeyote.

Timu hizi zimeshawahi kukutana mara nne huku Argentina wakiipiga Croatia mara mbili, Croatia wakipata ushindi mara moja na mara moja huku ya mwisho wakitoka bila suluhu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad