Mmiliki wa Jamii Forum Aachiwa Huru na Mahakama

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums, MaxenceMelo na Mwanahisa wa  mtandao huo, Micke William baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa aliwaachia huru washtakiwa hao leo Juni 1, baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka na kuona ushahidi huo hauna mashiko.

“Hakukuwa na ushahidi unaoeleza moja kwa moja wa barua hiyo ya kuwataka watoe taarifa za kampuni yao na ushahidi huo una mashaka?” amesema Mwambapa

Katika kesi hiyo Melo na mwenzake wanadaiwa kuzuia uchunguzi wa jeshi la polisi kwa kukataa kutoa taarifa za kampuni yao.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa,amedai kuwa baada ya usajili, kampuni hupewa taarifa za siri ambazo huwezesha mtu kuingia katika mtandao huo husika hivyo washtakiwa hao walikuwa na uwezo kuona taarifa kwenye mfumo wao.

Kishenyi amedai kuwa kufuatia jitihada hizo za Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum(ZCO) za kuwataka washtakiwa kutoa taarifa muhimu na wao kukataa walikamatwa na kufikishwa mahakamani.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad