Msukuma Ampa Makavu Waziri Sakata la Kupima Samaki Jikoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku Musukuma amemtaka Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhanga Mpina kujitafakari na kung’atuka kufuatia maofisa wa wizara hiyo kuingia bungeni bila ridhaa katika mgahawa wa Bunge na kupima samaki wanaodaiwa kuvuliwa haramu.

Musukuma ametoa kauli hiyo leo Jumatano Juni 20, 2018 bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2018/19.

“Nilikamatwa na samaki katika basi langu, tukaombwa rula…, waziri ajitafakari,” amesema Musukuma na kuongeza;

“Wizara hii  tumekuwa na mawaziri watano madaktari lakini leo tumeleta mgambo sijui shule ya aina gani? ni vizuri tukakaguliwa vyeti, mtu ana elimu ya kuunga uunga, yeye amekiri sijui hajui kwamba anakosea.

"Huu urais utakuja kututokea puani hasa sisi wasukuma, tumeamua kunyamaza na kumwachia Mungu apambane nae.”

Akitoa taarifa ya Serikali bungeni leo kuhusu kilichotokea jana, Mpina amesema ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za wizara ikiwamo operesheni sangara ambayo jana ilitendeka bungeni, itaendelea lakini kwa bahati mbaya utekelezaji huo haukuzingatia tararibu za Bunge.

Amesema Juni 19 akiwa katika mgawaha wa Bunge aliona samaki wa sato akahisi wapo chini ya sentimita 25 na kuagiza wachunguzwe.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad