Mtoto Anyongwa kwa Kuvunjwa Shingo Akiwa Anachunga Mifugo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtoto Anyongwa kwa Kuvunjwa Shingo Akiwa Anachunga Mifugo
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma, limewakamata watu wanaodhaniwa kumuua kwa kumnyoga kwa kumvunja shingo mtoto wa jamii ya kifugaji aliyetambulika kwa jina la Chanya Rugwashi (12).

Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Jemen Mushi, alisema  baada ya watu hao kutekeleza unyama huo, waliiba kondoo wawili na kuwachinja na kuondoka na nyama.

Kamanda Mushi alisema tukio hilo lilitokea Juni 20 katika eneo la mto Nampungu katika Kitongoji cha Matikiti Mashambani katika Kijiji cha Nambalapi.

Kamanda Mushi alifafanua kuwa marehemu Rugwashi alikutwa akichunga mifungo mingi wakiwamo ng'ombe, mbuzi na kondoo, lakini watu hao baada ya kufanya mauaji hayo waliiba kondoo wawili tu.

Kufuatia tukio hilo, Kamanda Mushi amewaomba wananchi ambao wanawafahamu watu waliotekeleza unyama huo kulisaidia Jeshi la Polisi ili kuwakamata haraka na kupisha vyombo vya sheria kutekeleza wajibu wake.

Kaka wa marehemu Rugwashi, Bundala Rugwashi, alisema kuwa mdogo wake alipotea Juni 20 na kwamba baada ya kubaini hali hiyo, walianzisha msako katika msitu huo na kufanikiwa kuupata mwili wake Jumamosi ukiwa umening'inizwa katika mti.

Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa kwa viongozi wa serikali ya Kata ya Masonya na baadae kituo cha polisi.

Taarifa ya uchunguzi wa mwili wa marehemu Rugwashi iliyotolewa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Tunduru, Dk. Vitaris Lusasi, inaeleza kuwa chanzo cha kifo hicho ni kuvunjika shingo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad