Mtoto wa Miaka 11 Afanyiwa Ukatili wa Kutisha Achomwa Moto Makalio na Kufungiwa Ndani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Na magdalena kashindye kahama
Mtoto mwenye umri wa miaka {11}amechomwa moto makalioni na kufungiwa ndani kwa muda wa siku mbili kwa kosa la kuiba pesa kiasi cha shilingi elf tano kitendo ambacho ni cha kikatili katika maisha yake .

Mtoto huyo   anayesoma darasa la tatu  katika shule ya msingi Mwinyi iliyopo mkoani Tabora jina limehifadhiwa  amefanyiwa ukatili huo siku ya jumatatu ya tarehe 11  /06 /2018 akiwa kwa baba yake mdogo wilayani kahama.

 Akizungumza na kituo hiki Mtendaji wa mtaa wa nyihogo Bwn.Antony Costa  amesema kuwa amepata taarifa kutoka kwa mwenyekiti pamoja na majirani wa familia hiyo na kuwa mtuhumiwa wa kosa hilo bado hajakamatwa

'Nilipata taarifa za tukio hilo kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa na majirani na ndiponilipofika eneo la tukio na mtuhumiwa hajakamatwa "alisema Costa. .….

Pia msemaji wa Dawati La Jinsia wilayani Kahama mkoani shinyanga Bi . Jenny Joakim Eras  amekili kupokea  tukio la mtoto huyo ofisi kwake na kuwa mtoto anaendelea na matibabu katika hospitali ya halmashauri ya mji wa kahama .

Eras  ametoa ushauri kwa wanajamii  kuwa na malezi bora kwa watoto woa kwa kuzingatia sheria ya mtoto ya mwaka 2009. .
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad