Serikali Yamtaka Prof. Jay Kufanya Jambo Hili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali Yamtaka Prof. Jay Kufanya Jambo Hili
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amemuagiza Mbunge wa Mikumi (CHADEMA) Joseph Haule ‘Prof. Jay’, kupeleka ushahidi kutokana na kuwa na madai ya kupotea watu 40 katika kata ya Luhembe, jimboni kwake.

Naibu Waziri Hasunga ametoa agizo hilo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mikumi lililohoji, kuwa anaomba ufafanuzi kwa serikali juu ya kupotea kwa watu 40 jimboni kwake na hawajulikani walipo na tabia ya watumishi wa TANAPA kuwachukua wakazi wa Mikumi na kuwatesa.

Akijibu swali hilo Hasunga amesema, "Mheshimiwa Mbunge naomba ulete ushahidi wa kupotea kwa wananchi ili kutanabaisha taarifa hizo na serikali itashughulikia suala hilo maana serikali ipo kwa kulinda usalama wa wananchi”.

Naibu Waziri ameongeza kuwa serikali tayari imetatua mgogoro wa mpaka kati ya wakazi wa Mikumi na maeneo ya hifadhi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad