Argentina Yatupwa Nje Kombe La Dunia, Mbappe amfanya kitu mbaya Messi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Timu ya Taifa ya Ufaransa imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia nchini Urusi jioni hii baada ya kuitungua Argentina ikiongozwa na kapteni wao, Lionel Messi kwa bao 4-3, mchezo uliokuwa mkali na wenye hisia miongoni mwa mashabiki.

Ushindi huo wa Ufaransa umechagizwa zaidi na Kylian Mbappe ambaye ametupia kambani mabao mawili huku akisababisha penati ya bao la kwanza.

Ufaransa walikuwa wa kwanza kufunga kunako dakika ya 13 kupitia kwa Antoine Griezmann kwa mkwaju wa penati baada ya Mbappe kufanyiwa madhambi ndani ya boksi kabla ya Angel Di Maria kusawazisha dakika ya 43. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Ufaransa 1-1 Argentina.

Kipindi cha pili, Argentina walianza na kasi ya ajabu ambapo dakika ya 48 walifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Gabriel Mercado.

Game ikawa ngumu kwa upande wa Ufaransa, lakini upepo ulibadilika  ambapo Benjamin Pavard alisawazisha na kufanya bao kuwa 2-2. Dakika ya 64, Kylian Mbappe akaandika bao la tatu kwa Ufaransa na kabla ya mchezaji huyo kuwamaliza na bao la 4 dakika ya 68.

Argentina walizinduka dakika za mwisho na kufunga bao la tatu kupitia kwa Sergio Aguero dakika ya 90. Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa, Ufaransa 4-3 Argentina.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad