Azam Yafunguka Siku ya Shabaan Idd Kutua Hispania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Azam Yafunguka Siku ya Shabaan Idd Kutua Hispania
Klabu ya soka ya Azam FC kupitia kwa meneja wake Phillip Alando, imesema mshambuliaji wao Shaaban Idd ambaye amesajiliwa na timu ya Tenerife ya Hispania, ataondoka nchini mara baada ya michuano ya Kombe la Kagame.


Mchezaji Shaaban Idd mwenye jezi nyeupe kwenye moja ya mechi za timu yake.

Akiongea leo na eat.tv meneja huyo amesema kila kitu kimeshawekwa sawa kati ya Azam FC na Tenerife FC, hivyo mchezaji huyo ataondoka hivi karibuni baada ya michuano ya Kombe la Kagame ambayo inaendelea hapa nchini huku Azam FC akiwa ndio bingwa mtetezi.

''Shaaban tayari ana mkataba wake na Tenerife na taratibu zote ameshakamilisha, kilichobaki ni kumaliza kuitumikia klabu yetu kwenye michuano ya Kagame kisha asafiri kwenda Hispania kwaajili ya kuanza maisha mapya ya soka la kimataifa'', amesema Alando.

Shaaban Idd anaungana na nyota mwingine wa Tanzania anayechezea timu hiyo, Farid Mussa. Alando ameongeza kuwa wao kama timu wataendelea kuendeleza vipaji hata kama timu hazitawanunua moja kwa moja lakini kwa vipaji vya nyota hao wataendelea kuwaruhusu wakacheze kwa mkop

Mshambuliaji huyo amesaini mkataba miaka 2 kucheza kwa mkopo ndani ya Tenerife. Msimu uliopita klabu ya Tenerife ilimaliza katika nafasi ya 11 kwenye ligi daraja la pili ya Hispania maarufu kama  'Segunda B' ambayo washindi watatu huwa wanapanda ligi kuu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad