BASATA Haiwezi Kunilipa Huko ni Kunichafua- Steve Nyerere

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BASATA Haiwezi Kunilipa Huko ni Kunichafua- Steve Nyerere
Msanii Steve Nyerere, amesema siyo kweli kuwa amepewa fedha na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ili aweze kuwashawishi wasanii wenzake juu ya mabadiliko mapya ya tozo yaliyotangazwa na baraza hilo siku za hivi karibuni ili wakubaliana nayo.

Steve amebainisha hayo wakati akizungumza na www.eatv.tv leo Julai 13, 2018 baada ya wadau mbalimbali wa filamu na muziki kumshambulia kupitia ukurasa wake wa kijamii kuwa amepatiwa fedha 'fungu lake' ndio maana anajifanya kutaka kukaa kikao na wasanii wenzake ili wapate ufumbuzi juu ya jambo hilo ambalo limekuwa gumzo kwa sasa.

"BASATA haiwezi kunipa fedha 'fungu' lolote kwa ajili yangu mimi huko ni kuichafua, mimi ni nina nguvu gani mpaka wanilipe. Lazima niwe upande wa wenzangu ambao ni wasanii na msema ukweli siku zote ni mpenzi wa Mungu, kiukweli milioni tano kwa msanii ni pesa nyingi sana hata ingekuwa milioni moja bado shida ingekuwepo", amesema Steve

Pamoja na hayo, Steve ameendelea kwa kusema "kama kweli BASATA walitaka kutusaidia walipaswa waanze kutupa kazi wao kwa kututengenezea mifereji ya kupata matangazo ili ndio watake hizo pesa walizozitaka. Kwa namna moja ama nyingine hayo makampuni yakikataa kutupa matangazo sisi na yakaenda kuwapa raia wa kawaida hao BASATA watakuwa wanapata nini zaidi ya hasara tu. Duniani kote msanii anapata fedha kupitia matangazo".

Mbali na hilo, Steve Nyerere ameitaka jamii kutoliingiza suala hilo katika mlango wa kisiasa licha ya kuwa yeye yupo ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM).

Siku za hivi karibuni Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) liliweza kufanya mabadiliko mbalimbali katika tozo zao za utoaji wa huduma ikiwemo ya makampuni kulipa milioni tano kwa BASATA endapo watamtumia msanii kufanya tangazo la aina yoyote, jambo ambalo limekuwa likipingwa na wasanii wengi nchini wakidai kuwa kwa kitendo hicho watakosa kazi.

Kupitia kipindi cha Planet Bongo kilichorushwa Julai 10, 2018 na  East Africa Radio, BASATA ilitoa ufafanuzi juu ya suala hilo kuwa sio kweli kwamba msanii anatakiwa kulipa milioni 5 akifanya tangazo bali kampuni husika ndio inapaswa kufanya hivyo kwa kuwa wanaingiza kipato kikubwa kutumia tangazo hilo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad