Kagere Awapa Onyo Kali Wanaomwita Babu " Wekeni Akiba ya Maneno Subirini Ligi Ianze"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kagere Awapa Onyo Kali Wanaomwita Babu " Wekeni Akiba ya Maneno Subirini Ligi Ianze"
MSHAMBULIAJI wa Simba, Medy Kagere, amesema wanaomuita 'mzee' waweke akiba ya maneno kwa kuwa atawashangaza kwenye michezo ya Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.


Kagere, alisema ameyesikia maneno ya baadhi ya mashabiki wa timu pinzani kuwa Simba imemsajili huku umri wake ukiwa umekwenda, lakini amesisitiza ana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu hiyo.

"Nimezeeka au umri mkubwa hayo ni maneno ya mashabiki tu, nipo Simba kwa ajili ya kufanya kazi na sitowaangusha, wanaosema hivyo wasubiri ligi ianze," alisema Kagere.

Kagere, alisema alitamani kuona timu yake inatwaa ubingwa wa Kombe la Kagame, lakini kwa bahati mbaya hawakufanikiwa kufanya hivyo.

"Ndio matokeo ya mpira, tulipambana sana kwenye mchezo ule na Azam, lakini hatukuwa na bahati sasa tunajipanga kwa ajili ya ligi," alisema Kagere.

Kagere, ambaye amemaliza michuano hiyo akiwa na mabao manne, alifunga bao moja wakati Azam ikishinda 2-1, na kisha kuonyeshea mashabiki ishara ya babu anayetembelea mkongojo, akimaanisha bado ana uwezo.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad