Trump Ayataka Mataifa ya NATO Kuongeza Bajeti ya Ulinzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Trump Ayataka Mataifa ya NATO Kuongeza Bajeti ya Ulinzi
Rais Donald Trump amewataka washirika wa NATO kuongeza kiasi cha fedha mara mbili zaidi kwaajili ya kuongeza bajeti ya ulinzi ambayo kwa sasa wanachangia asilimia mbili tu,na yeye akiwataka kufikia mchango wa asilimia nne kutoka kwenye pato la mataifa hayo. Hata hivyo pamoja na kuhimiza ongezeko amezitaka nchi hizo kulipa ahadi zao za asilimia mbili mara moja.

Pamoja na rais Trump kuhimiza washirika hao wa NATO kuwa na ongezeko la bajeti ya ulinzi,lakini mataifa hayo yamesema hayawezi kutimiza ahadi zao ifikapo mwaka 2024.

Katika hatua nyingine Trump ameilaumu Ujerumani kwa madai kwamba inatumia kiasi kidogo, katika bajeti ya ulinzi wakati ambapo inatumia fedha nyingi katika ununuzi wa bidhaa za nishati, kutoka nchini Urusi,taifa ambalo walipa kodi wa Marekani wanachangia kodi zao kukabiliana na vitisho vyake.

Kansela wa Ujeruman Bi Angela Merkel,amejibu shutuma hizo za Trump na kudai idadikubwa ya wanajeshi wake wapo katika vikosi vya NATO

Bi Merkel Anasema "sisi ni taifa la pili kuwa na kikosi kikubwa cha wanajeshi wetu,tunanatoa mchango mkubwa kijeshi kwa NATO na kushiriki kwa kiwango kikubwa kule Afghanistan,kulinda hata maslahi ya Marekani kwa sababu ya ushiriki wao Afghanstan,jambo ambalo ni mfano wa kuiunga mkono Marekani, kwa mjibu wa kifungu namba tano cha NATO'' Bi Merkel.

Hata hivyo katika mkutano wao wa pamoja na waandishi wa Habari na Bi Angela Merkel,Trump ameonekana kubadili msimamo wake na kuwa na kauli za kuiunga mkono Ujerumani.

"Tumekuwa na mkutano mzuri,tunajadili matumizi ya kijeshi,tunazungumza kuhusiana na biashara.Tuna uhusiano mzuri sana na Kansela na uhusiano mzuri na Ujerumani. Tunaamini kuwa tunafikia mafanikio makubwa sana,na biashara yetu itakua,na mambo mengine mengi yataongezeka.Lakini tunasubiria na kuona nini kinatokea miezi michache ijayo".

Mkutano wa Brussels unakuja ikiwa ni takribani wiki moja tu kabla ya Rais Trump kuwa na mkutano wa kwanza na rais wa Urusi Vladmir Putin mjini mjini Helsinki nchini Finland.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad