Ukiwa Hauna Maamuzi kwa Mke Wako ni Jambo Jema

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abubakar Chande maarufu kama 'Dogo Janja' ambaye pia ni mume wa msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amedai katika ndoa yao yeye ndio mwanaume na mwenye sauti ya kutoa maamuzi ya jambo lolote tofauti na watu wanavyomfikilia.


Dogo Janja amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE 'FNL' inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya kuwepo kwa tetesi za kipindi kirefu zilizokuwa zinadai Janjaroo hana maamuzi yoyote katika ndoa yake kwa kuwa mwenye sauti ya kuamua jambo lolote ni mke wake Irene Uwoya.

"Ukiwa hauna maamuzi au sauti kwa mke wako wa halali ni kitu kizuri sana tofauti ukiwa hauna sauti kwa hawala. Mimi nina mtii mke wangu naye pia anafanya hivyo, kwenye ndoa yangu nina simama kama baba", amesema Dogo Janja.

Pamoja na hayo, Dogo Janja ameendelea kwa kusema
"watu wengi wanachukulia mambo kwa juu juu tu kwa mzaha, mimi nina sauti kwa mke wangu ninaweza kumwambia leo usitoke na huwa atoki au asifanye kitu fulani na akanisikiliza, 'so' sio kila jambo nitakalo mkataza basi nitangaze ila mpaka mke wangu akifanya jambo fulani mjue nina taarifa nayo na ninaelewa. Ndoa ni taasisi kubwa sana tofauti na watu ambao wapo tu mtaani wanatoa maamuzi yao bila ya kuelewa".

Kwa upande mwingine, Dogo Janja amedai watu wengi wamekuwa wanaongelea kuhusiana na ndoa yake kwenye mitandao ya kijamii bila ya kuwa na ufahamu wa aina yoyote juu ya taasisi hiyo ambayo ina uwanja mpana ndani yake.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad