Viatu Virefu Vyamuumbua Wema Sepetu Morogoro

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Viatu Virefu Vyamuumbua Wema Sepetu Morogoro
STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu ametengeneza kichwa cha habari mjini Morogoro baada ya juzikati kujikuta akiumbuka kufuatia viatu alivyokuwa amevaa kutaka kumng’oa meno alipokuwa akipanda jukwaani.



Kisanga hicho kilimpata Wema alipotinga kwenye mashindano ya Miss Morogoro 2018 ambapo alialikwa kama mmoja wa majaji. Awali saa 6 usiku wakati Wema akiingia katika Ukumbi wa

Hoteli ya Morogoro lilipofanyika shindano hilo alionekana akiwa amevalia gauni refu la rangi ya gold huku chini akiwa ametinga viatu virefu vilivyompa wakati mgumu kutembea kwa mikogo. Hata hivyo staa huyo alifanikiwa kufika kwenye meza iliyoandaliwa kwa ajili ya majaji na kukaa lakini shughuli ilikuwa pale ambapo alitakiwa kupanda jukwaa kutoa neno.



Wakati akielekea kwenye ngazi za kupandia jukwaani, Wema alionekana kuyumba na kutaka kupiga mwereka lakini mmoja wa watu waliokuwa karibu yake waliwahi kumzuia na ndipo aliposhikiliwa na kupandishwa. Hata hivyo, hali iliendelea kuwa tete baada ya staa huyo kufika ngazi ya pili ya jukwaa ambapo aliyumba tena na ndipo mtangazaji wa Redio Planet FM ya Moro, Warda Makongwa akaongeza nguvu na kumfikisha jukwaani salama.



Wakati wa kushuka ili kumuepushia aibu staa huyo, wadada wawili walionekana kumshika mikono na kushuka naye taratibu huku mtangazaji wa Redio Clouds FM, Gardner G Habash naye akiongeza nguvu. Mbali na viatu kumuumbua Wema, umbo lake namba nane lililokuwa limejengeka vilivyo kutokana na gauni alilokuwa amevaa lilikuwa gumzo na wengi waliibua gumzo kutokana na msambwanda wa mrembo huyo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad