Baada ya Mkuu wa Mkoa Mbeya Kung'ang'ania Vyeo Viwili CCM Kumaliza Utata Huo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya Mkuu wa Mkoa Mbeya Kung'ang'ania Vyeo Viwili CCM Kumaliza Utata Huo
Baada ya kuwepo kwa mkanganyiko juu ya Mkuu mpya wa mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila kushika nyadhifa mbili ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, CCM imesema suala hilo litaamuliwa na Kamati Kuu ya chama hicho.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Ndugu Humphrey Polepole ameongea na www.eatv.tv na kueleza kuwa kila kitu kipo kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho hivyo suala la Albert Chalamila kuwa na kofia mbili litaamuliwa kwenye mkutano wa kamati kuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

''Kanuni ya uchaguzi ya CCM inaeleza bayana mtu mmoja kofia moja, lakini pia kanuni imetoa mamlaka kwa kamati kuu ya chama kumwezesha mtu mmoja kushika kofia mbili endapo itaona inafaa na kamati chini ya Mwenyekiti Ndugu Magufuli itakaa hivi karibuni na itaamua kama aendelee na kofia zote au moja'', - amesema.

Chalamila aliteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli pamoja na viongozi wengine wa mikoa na wilaya ambapo jana kupitia mkutano wake na viongozi wa dini mkoa wa Mbeya aliweka wazi kuwa hawezi kujiuuzulu uenyekiti wa wa CCM mkoa wa Iringa labda apokee maelekezo kutoka kwa Rais ambaye amemteua.

Chalamila sio kiongozi wa kwanza wa CCM kuwa na kofia mbili ambapo alitanguliwa na wengine kama Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi aliyeteuliwa na Rais Magufuli mwaka 2016 kuwa mkuu wa mkoa huo huku akiwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya. Hata hivyo, katika uchaguzi wa chama hicho mwaka jana, Zambi hakutetea kiti chake.

Kiongozi mwingine ambaye amewahi kushika nyadhifa mbili ni mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Musukuma’ ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Geita ambaye naye hakutetea nafasi hiyo katika uchaguzi wa mwaka jana
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad