BASATA Wafunguka Ishu ya Kumtaka Diamond Alipie Kibali cha Kuhudhuria Birthday ya Tiffah SA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BASATA wafunguka ishu ya kumtaka Diamond alipie kibali cha kuhudhuria birthday ya Tiffah SA
Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limekanusha taarifa zilizosambaa mtandaoni kwamba wamemtaka Diamond kwenda kulipia kibali cha kusafiri kwenda Afrika Kusini kwenye birthday ya mtoto wake Tiffah.

Diamond akiwa na mtoto wake Tiffah.

Hatua hiyo imekuja baada ya wiki moja iliyopita baraza hilo kutangaza sheria mpya zinazowakata wasanii kuomba vibali wanapotaka kwenda nje ya nchi kwaajili ya show zao.

Basata wamesema sio kweli kwamba wamemtaka Diamond kuchukua kibali cha kwenda kuhudhuria birthday ya mtoto wake kama inavyoadiwa katika mitandao ya kijamii.

“Tunapenda kuutarifu umma kuwa taarifa inayosambaa kwamba Msanii Diamond anatakiwa kuchukua kibali BASATA kwenda kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa mwanaye si ya kweli,” wameandika Basata kupitia mtandao wao.

Waliongeza “Vibali vya wasanii kwenda nje havihusiani na safari binafsi. Tunazidi kuwakumbusha wasanii kufuata taratibu zote wanapoenda kufanya maonesho nje ya nchi.,”

Wiki moja iliyopita muimbaji huyo alizuiwa na Basata kwenda kufanya show nje kwa kuwa hakuchukua kibali cha kwenda kufanya show nje ya nchi lakini baadae aliweza kufuata taratibu za kuchukua na kusafiri.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad