Deusdedit Kakoko Athibitishwa Kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bandari

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Deusdedit Kakoko Athibitishwa Kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bandari
Aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Deusdedit Kakoko amethibitishwa  kuwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo.

Akizungumza na wafanyakazi wa TPA jana Ijumaa Agosti 10, 2018 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema amechukua uamuzi huo kutokana na utendaji kazi wake.

Amesema ni kawaida watumishi wa Serikali wanapoteuliwa kwenye nafasi kama hizo kukaimu ili kuangalia utendaji wao wa kazi na kama akiiridhisha mamlaka anathibitishwa.

“Kipindi  alichokaimu ameangaliwa na Serikali na bodi ya TPA kwa bahati nzuri bodi imenipa taarifa yake ya utendaji leo na nimemthibitisha,” alisema.

"Tafadhali tembo usilitie maji, nimekupandisha kwa sababu nimeona utendaji wako nina imani na wewe, usiniangushe.”

Kamwelwe alisema kuwa kuna wakati huwa anamuhurumia kutokana n kutumia muda mwingi kazini.

"Huwa nampigia simu hata saa nne  usiku na bado anakuwa yupo ofisini hadi namuuliza huwa unalala kweli. Watu kama hawa ndio tunawataka na wengine igeni mfano wake, kazi zinafanyika saa 24 ziendelee vivyo hivyo,” alisema.

Kwa upande wake, Kakoko alisema hatamuangusha waziri huyo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad