Inasikitisha Mtoto wa Miaka 8 Abakwa na Kusababishiwa Fistula

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Inasikitisha Mtoto wa Miaka 8 Abakwa na Kusababishiwa Fistula
Mwanafunzi  wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka minane mkoani Manyara, anadaiwa kubakwa na mkazi mmoja wa wa Kijiji cha Maganjwa wilayani Babati na kumsababishia   ugonjwa wa fistula.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Dareda,  Joseph Lorri,  alithibitisha kupokewa mtoto huyo ambaye alikuwa na hali mbaya ikiwamo kuvuja damu kutokana na majeraha ya kuchanika sehemu za siri ikiwamo haja ndogo na kubwa.

Alisema mtoto huyo alipokewa hospitalini hapo Julai 16, mwaka huu saa 3.30 usiku akiwa ameharibiwa sehemu zake za siri na anavuja damu na kutokwa nyama sehemu zake za  siri.

“Tukio lenyewe linavyoelezea mtoto huyu alibakwa, na mtoto alimtaja aliyembaka ambako jamii ilikuwa ikimtafuta mbakaji huyo.

“Alivyoletwa alikuwa anatoka damu sehemu za siri na kulikuwa na mpasuko wa kidonda  kwenye sehemu ya haja kubwa na ndipo tukaanza kumfanyia vipimo,” alisema Dk. Lorri.

Alisema mtoto huyo alitibiwa kwa kufanyiwa upasuaji  na kushonwa kuunganisha sehemu hizo zilizochanika na kwamba hadi sasa hali yake inaendelea vizuri kwa uangalizi wa madaktari wa hospitali hiyo.

“Tunaendelea na jitihada za kumtibu lakini pi tumemwanzishia matibabu ya dawa za kumkinga dhidi ya maambukizi ya virusi  kutokana na tukio lenyewe jinsi lilivyokuwa,” alisema
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad