Okwi Mambo Yamuendea Hovyo Leo Kuikosa Mechi Yao Dhidi ya Mbeya City

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Okwi Mambo Yamuendea Hovyo Leo Kuikosa Mechi Yao Dhidi ya Mbeya City
MAMBO yamekwenda ndivyo sivyo kwa straika wa Simba, Emmanuel Okwi ambaye alionekana anaweza kuwa fiti kucheza leo lakini hali yake imebadilika na hatacheza dhidi ya Mbeya City leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Okwi aliumia hivi karibuni katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.



Alionekana kuweza kuiwahi Mbeya City lakini juzi Jumamosi uongozi wa benchi la ufundi la Simba unaoongozwa na Mbelgiji, Patrick Aussems, ulilazimika kumpatia muda wa mapumziko mshambuliaji huyo kutokana na kushindwa kufanya mazoezi.

Uongozi huo ulifikia hatua hiyo baada ya Okwi kudai kuwa anahisi maumivu makali ya kiuno, jambo ambalo lilimfanya ashindwe kufanya mazoezi kama ilivyo kawaida yake.



Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba ambazo Championi Jumatatu limezipata zimedai kuwa hali hiyo ililimfanya Aussems pamoja na daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe kumpeleka hospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo lakini pia akataka Okwi kuwa nje ya uwanja mpaka hapo atakapokuwa amekaa sawa.



“Jana (juzi) alifanyiwa vipimo kwa dokta mmoja hivi ambaye ni mtaalamu wa viungo na majibu yake yatatoka leo (jana) ili kujua ni nini kinachomsumbua zaidi ili aweze kupata matibabu.

“Lakini pia kama vipimo havitaonyesha tatizo lolote basi atatakiwa kupmzika kwa muda ili aweze kuwa sawa, kwa hiyo kuanza sasa hatafanya mazoezi tena mpaka hapo kocha atakapojiridhisha kuwa hana tena maumivu na yupo sawa,” kilisema chanzo hicho cha habari.



Alipotafutwa Okwi ili aweze kuzungumzia hilo, hakupatikana kama ilivyokuwa kwa dokta wa timu hiyo Yassin Gembe lakini meneja wa timu hiyo, Richard Robert alijibu kwa kifupi: “Bado hajakaa sawa ila maendeleo yake siyo mabaya na anaendelea kupata matibabu.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad