Shilole Awatolea Uvivu Wanaomponda Baada ya Kuomba Msaada kwa Rais Mgufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Shilole Awatolea Uvivu Wanaomponda Baada ya Kuomba Msaada kwa Rais Mgufuli
Msanii wa bongo fleva na mjasiriamali nchini, Shishi Baby amefunguka na kudai yeye sio mtu wa ku-fake maisha kama baadhi ya watu wanavyomfikiria mitandaoni, huku akiwaomba radhi kwa wale ambao wamekwazika kwa yeye kuomba msaada kutoka kwa Rais Magufuli juu ya watoto wake.

Shilole ametoa ufafanuzi huo leo asubuhi kupitia ukurasa wake wa kijamii baada ya kuenea 'video clip' iliyokuwa ikimuonyesha akiongea lugha ya ughaibuni 'kiingereza', akimualika Rais Dkt. John Magufuli kuhudhuria katika mgahawa wake ili kusudi aweze kuonja mapishi yake pamoja na kuomba msaada wa watoto wake katika kupata elimu bora.

"Niombe radhi kwa mlionielewa tofauti mimi huwa si-fake maisha naishi maisha yangu, sina utajiri huo kama mlivyonisema hata nyumba niliwaambia nimejenga kwa kujiwekea kidogo kidogo kama mama ntilie na mwanamuziki, ndio maana nilipofikia hatua fulani nikaona ni vizuri ku-share na nyie ili muone nguvu ya 'support' yenu inavyonipa maendeleo",ameandika Shilole.

Pamoja na hayo, Shilole ameendelea kwa kusema "nilichokiomba juzi kwa baba Magufuli ni 'support' na ufadhili wa wanangu kuendelezwa katika vipaji na taaluma wanazopenda kusoma. Mimi napambana sana kuwasomesha lakini pia natamani wapate kitu zaidi ya nachoweza kuwapatia, hivyo nikaona ni kwanini nisiweke kilio changu kwa Mheshimiwa kwasababu elimu kwa watoto wa kike ni moja ya mambo ambayo naamini anayasimamia vema".

Mbali na kauli hizo, Shilole ni miongoni mwa wasanii wa kike nchini wanaopambana usiku na mchana, katika kuhakikisha anajipatia riziki kupitia maarifa aliyokuwa nayo na nguvu zake na kumfanya awe tofauti na wanawake wengine ambao wamekuwa wakisubiria pesa za mahitaji kutoka kwa wanaume zao.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kuna watu wengi wanahitaji support kwa watoto wao lakini sio mpaka kwa Magufuli na kuna watu wengi sana wana migahawa lakini hawamsumbui Magufuli aache majukumu yake ya kazi ili aende kwenye migahawa yao

    ReplyDelete

Top Post Ad