Sijamsajili Alikiba sababu ya kuimba sana –Kocha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sijamsajili Alikiba sababu ya kuimba sana –Kocha
Kocha mkuu wa klabu ya Coastal Union ya Tanga, Juma Mgunda, amefunguka juu ya kiwango cha mchezaji mpya wa klabu hiyo, AliKiba katika mazoezi yake ya kwanza tangu ajiunge nayo msimu huu.


Alikiba yupo mkoani Tanga na Ijumaa, Agosti 3, amehudhuria mazoezi ya klabu hiyo ikiwa ni katika maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajia kutimua vumbi, Agosti 22.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa programu ya mazoezi hayo, kocha Mgunda amesema .

“ Alikiba mimi nimemsajili kwasababu nimemwona anajua kucheza na wala sikumsajili Ali kwasababu anaimba sana, kwahiyo nataka ule uwezo wake wa kucheza ndiyo maana nikazungumza naye nikamshawishi akaniambia mwalimu nitafikiria na kweli akafikiria akaniambia niko tayari kucheza “.

Pia amewataka mashabiki wa Coastal Union na wadau wa soka nchini kuondoa wasiwasi juu ya mchezaji huyo na kwamba wategemee mambo mazuri kutoka kwake.

Coastal Union imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Alikiba, mkataba ambao unamruhusu kufanya kazi yake ya awali ya kimuziki kama kawaida na kuruhusiwa kucheza pale anakuwa hana majukumu mazito.

Klabu hiyo iliyopanda ligi kuu msimu huu baada ya kushiriki  kwa mara ya mwisho msimu wa 2015/16, itaanza kampeni ya ligi kuu Tanzania bara, Agosti 22 itakapowakaribisha ‘Wanapalohengo’ Lipuli Fc ya mkoani Iringa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad