Siwezi Kuacha Muziki Labda Kifo Kitutenganishe- Joh Makini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Siwezi Kuacha Muziki Labda Kifo Kitutenganishe- Joh Makini
Siku ya jana ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya rapa kutoka kundi la Weusi, Joh Makini ambapo alipata fursa katika kituo cha redio cha East Africa Radio na kufunguka kama aliwahi kufikiria kuacha muziki na kufanya ishu zingine.


Joh amedai haitokuja kutokea maishani mwake, kuacha kurap labda kifo ndio kiwe sababu ya yeye kumtenganisha na muziki.

“Kufanya vitu vingine tofauti katika maisha hilo ni muhimu kabisa, lakini kufikiria kuacha muziki sijui, kwasababu na kuwa mzito sana kusema itafikia siku ntashindwa kurap ?, sijui ila napenda muziki sana”, amesema Joh Makini.

Aliongeza “Endapo ikitokea nikiacha kurap na kutoenda studio lazima ntakuwa kwenye mzunguko wa kufanya vitu vingine na muziki pia. Sioni sababu ya kuacha muziki labda kifo ndio kitanitenganisha lakini sio kitu kingine”.

Wasanii wengi wanakuwa kwenye wakati mgumu pindi wanapoulizwa kuhusu kuachana na muziki, kutokana na baadhi yao kufanya muziki kama kazi na starehe hivyo kuwawia vugumu kuachana na vitu hivyo kutokana na mazoea.

Mbali na hilo, Joh Makini amesema kwa sasa muziki wa hiphop nchini unalipa kwa kiasi kikubwa, tofauti na ulivyokuwa zamani huku akiwarushia dongo wasanii wanaolalamikia kuwa yawezekana wao wenyewe hawajajipanga katika kutoa kazi nzuri ndio maana wanayumba.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad