Kauli ya Asia Baada ya Kushindwa Ukonga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kauli ya Asia baada ya kushindwa Ukonga
Aliyekuwa Mgombea Ubunge wa (CHADEMA) jimbo la Ukonga Asia Msangi ametoa kauli yake ya kwanza kuwa alitegemea kushindwa uchaguzi huo ikiwa ni saa chache tangu Msimamizi Mkuu wa uchaguzi wa Jimbo hilo kumtangaza Mwita Waitara kuwa mshindi wa jimbo hilo kwa kura 77795.

Akizungumza na www.eatv.tv Asia Msangi ameeleza alipokea taarifa kuwa angeshindwa uchaguzi huo kutoka kwa wapiga kura wake kwa kile alichokidai kuhujumiwa katika baadhi ya vituo vya kura ikiwemo kuzuiliwa kwa mawakala wake huku zoezi la kupiga kura likiwa linaendelea.

“…ulimwengu wote umeona mambo yaliyofanyika Ukonga, kwa sababu hata kabla ya uchaguzi nilipokea taarifa kuwa Asia hutoshinda.., wameamua kumuweka yeye (Waitara) ndio mbunge wacha wamuweke lakini Ukonga wameona anaewafaa ni nani? . wengi walinipigia simu kwamba hawapigi kura kwa sababu mawakala wangu waliwasumbua tangu saa 12 asubuhi.”

Uchaguzi huo ulihusisha wagombea 14 akiwemo Murshidi kabilinga (NRA) aliyepata kura 6, Kimosa Mohamed (UMD) kura 16, Rajabu Rashindi (NLD) kura 16, Mbwana Kibanda (UPDP) kura 17, Ngubi Ramadhani (ADC) kura 17, Kuzenga Faustine (UDP) kura 23, Kiambo Richard (CCK) kura 74, Nelbert Obatia wa NCCR-Mageuzi kura 27, Kisena Lucas (SAU) kura 40, Rehema Nasoro Chama cha Wakulima  91, Salama Masoud  (CUF) kura 405, Asia Msangi wa CHADEMA  kura 8676 na Mwita Waitara wa CCM kura 77795.

Kwa mujibu Msimamizi wa Mkuu wa uchaguzi jimbo hilo lilikuwa na wapiga kura 300,609 lakini waliojitekeza ni wapiga kura 88,270 tu ambao ni sawa na asilimia 29 ya wapiga kura waliojiandikisha.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hvi hata kwa akili ya kawaida tu ulitarajia ushinde? unatufanya wanaUkonga hatujui kilicho bora ebo!

    ReplyDelete
  2. kwanza....!!!!!
    hata hiyo pesonaliti unayo?....
    ebu jiangalie picha yako na ya waitara, hala wewe mwenyewe utoejibu utamchgua nani....???
    nasikia tetesi kuwa kura yako iliharibika...kwa kuwa mwanzo ulijipigia halafu ukabadili
    maawazo na kumpigia mwita.
    haya tuujuze kishtobe...

    ReplyDelete
  3. kabla yote kwanza....!!!!!
    hata hiyo personality unayo?....
    hebu jiangalie picha yako na ya Mwita, halafu wewe mwenyewe utoe jibu ukiambiwa utamchgua nani....???
    nasikia tetesi kuwa kura yako iliharibika...kwa kuwa mwanzo ulijipigia halafu ukabadilisha na kumpigia Waitara.
    haya tuujuze kamandia...

    Mta pata tabu sana hapo sakozi.

    ReplyDelete
  4. umependeza nywee zako...!!!
    na blouzi ime mechi...Amazing

    ReplyDelete

Top Post Ad