Kocha wa Simba Pasua Kichwa..Akataa Nyumba ya Kupanga..Ataka Kuishi Hotelini tu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, amezungumza na uongozi wa timu hiyo kuwa anataka kuendelea kukaa hotelini kwa kuwa amezoea na pia hajui kupika.

Aussems Jana Jumamosi aliiongoza timu hiyo kucheza dhidi ya Ndanda katika mchezo wa Ligi Kuu Bara na kutoka sare bila ya kufungana ukiwa ni wa tatu kwake na wa kwanza wa ugenini katika ligi ya msimu huu.

Ikumbukwe, Mbelgiji huyo alifikia katika Hoteli ya Golden Tulip ya Masaki kabla ya kuhamishiwa katika Hoteli ya Sea Scape iliyopo Mbezi Beach mara baada ya kuanza kazi kwenye timu hiyo na japo hulipa chumba Sh 170,000 kwa siku.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Aussems alisema hawezi kukubali kuishi kwenye nyumba za kupangiwa kwa kuwa maisha yake ya ukocha amekuwa akiishi hotelini.

“Kwa hapa ndiyo sehemu ambayo nitaendelea kuishi kwa muda wote, nilishawaambia viongozi na hilo wanalijua hivyo siwezi kwenda kuishi kwenye nyumba yoyote zaidi ya hapa.
“Unajua kwanza sijui kupika halafu maisha ya hotelini nimeyazoea tangu nimeanza kufanya kazi Afrika nimekuwa nikiishi hoteli sawa na hapa na uzuri huwa sichagui chakula ili mradi kiwe kitamu,” alisema Aussems.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad