Pale Mapenzi Yanapokuwa Moto Moto Hadi Kuchora Tatoo Mwisho wake Kuwa Makovu... Hawa Ndio Mastaa Waliobaki na Makovu ya Tatoo za Wapenzi Wao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Pale Mapenzi Yanapokuwa Moto Moto Hadi Kuchora Tatoo Mwisho wake Kuwa Makovu... Hawa Ndio Mastaa Waliobaki na Makovu ya Tatoo za Wapenzi Wao
MAPENZI ni kikohozi kukificha huwezi! Na siku zote unapopenda unaweza kufanya lolote ili tu umfurahishe yule uliyenaye aone tu thamani yako au umuhimu wa kuwa na wewe.  Kwenye mapenzi kuna sarakasi nyingi ambazo wawili mnaweza kupitia zikiwemo za furaha au huzuni. Mapenzi huwa machungu pale mnapochokana au kukinaiana na kulazimika kufikia mwisho wa ninyi wawili ambapo kwa aliyeachwa huwa na maumivu makali huku majuto yakiwa ni makubwa kwa kuwa anakumbuka yale yote aliyoyafanya kwa ajili ya mwenzake, lakini mwisho akaambulia kuachwa au kuachana.

Hata katika ulimwengu wa mastaa hali hii inawatokea wengi kwa sababu nao ni binadamu, wana hisia na wanapenda ambapo katika makala hii tunakuletea baadhi yao ambao walikuwa katika mapenzi mazito, wakajichora na majina ya wapenzi wao (tattoo) mwilini mwao kudhihirisha upendo wao, lakini mwisho penzi likapukutika.

CASTO DICKSON NA TUNDA

Huyu ni mtangazaji wa Clouds TV ambaye alikuwa kwenye mapenzi motomoto na mrembo Tunda Sebastian ambapo aliwahi kutangaza kuwa ndiye mkewe mtarajiwa na wanatarajia kufunga ndoa. Casto, kutokana na kwamba alikuwa kwenye penzi zito na Tunda aliamua kujichora jina la mwanadada huyo kwenye mkono ili kudhihirisha upendo wake, lakini hivi karibuni penzi hilo limevunjika baada ya Tunda mwenyewe kukiri licha ya mtangazaji huyo kukataa.
Related image
SHILOLE NA NUH MZIWANDA
Mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ alijichora tattoo ya jina la aliyekuwa mwandani wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kwenye kifua baada ya mpenzi wake huyo kumchora jina lake kwenye mkono hivyo naye ili kuonesha upendo akafanya hivyo.

Shilole alimwagana na Nuh na sasa ni mke wa ndoa wa Ashraf Uchebe ambapo baada ya kuachana na mwanamuziki huyo aliifuta tattoo hiyo kwa kuchora mchoro mwingine juu yake. Vivyo hivyo kwa Nuh, baada ya kuachana na Shilole aliifuta tattoo ya jina lake kwa kuchora mchoro mwingine juu yake kwani hazifutiki.
Image result for brown na wolper
BROWN NA WOLPER

Mwanamitindo huyu anayejulikana kwa jina la Barnaba Shelukindo ‘Brown’ aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper, lakini baadaye walimwagana.

Katika penzi lao, kutokana na kwamba Brown alimpenda Wolper aliamua kujichora tattoo ya jina lake kifuani ambapo baada ya penzi kuota mbawa aliifuta kwa kuchora ua juu yake kufuatia kuwa kwenye uhusiano na msanii mwingine wa filamu, Salma Jabu ‘Nisha’.NAWAL NA NUH

Huyu alikuwa ni mke wa ndoa wa mwanamuziki, Nuh Mziwanda, lakini ndoa yao ilivunjika wakiwa na mtoto mmoja.

Enzi za penzi lao, Nawal alijichora tattoo ya jina la Nuh Mziwanda kwenye mkono, lakini baada ya kuachana aliifuta na kubaki na kovu au inaonekana kama uchafu.
Image result for amber lulu tottoo ya young d
AMBER LULU NA YOUNG D

Amber Lulu ni msanii wa Bongo Fleva ambaye jina lake halisi ni Lulu Euggen, alijichora tattoo ya jina la aliyekuwa mpenzi wake, David Genz ‘Young D’ kwenye bega, lakini baada ya kumwagana aliifuta na kuchora ua lingine juu yake.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad