Sakata la Uchawi Zari Amfariji Hamissa Mobetto kwa Stairi Hii

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sakata la Uchawi Zari Amfariji Hamissa Mobetto kwa Stairi Hii
Kwa mara ya kwanza, mzazi mwenzake Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amevunja ukimya na kuamua kumfariji ‘mke mwenzake’ Hamisa Mobeto baada ya watu kumshambulia mitandaoni.



Kupitia ukurasa wake wa Instagram, jana Zari aliweka ujumbe ulioshiria kumfariji Mobeto bila kumtaja jina na ndipo watu walipojiongeza kwa kusema, amemfariji mrembo huyo kutokana na sakata lake la kuvuja kwa sauti iliyosikika akizungumza na mganga ili amroge mzazi mwenzake Diamond.



“Usiwape nguvu watu ya kukulinganisha wewe na watu wengine, kama hawawezi kuamua, waamulie, songa mbele na usigeuke nyuma, nenda mahali kwenye furaha, hakuna sababu ya kumuelezea kila mtu kwani safari ni yako, hakuna anayeelewa zaidi yako, hakuna cha kupeleka zaidi ya upendo kwa dada yangu wa Tanzania, futa machozi na hilo lipite,” aliandika Zari kwa lugha ya kingereza.


Risasi Jumamosi lilimvutia waya Zari ambapo alipopatikana alithibitisha kuwa ujumbe huo alimtumia Mobeto na kusema amefanya hivyo kiroho safi.

“Tunapaswa kusambaza upendo kwa sababu baadhi ya watu wanahitaji kutiwa moyo,” alisema Zari.



Wawili hao kwa nyakati tofauti wamezaa na staa wa Bongo Fleva, Diamond. Zari amezaa naye watoto wawili na kuachana naye huku Mobeto akizaa naye mtoto mmoja, ambapo pia wamemwagana.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad