Tiwa Savage Akimbiwa na Promota Ashindwa Kulipa Ghalama ya Hoteli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tiwa Savage Akimbiwa na Promota Ashindwa Kulipa Ghalama ya Hoteli
Mwanamuziki nyota mwenye asili ya Nigeria Tiwa Savage amelalamika na kudai aliachwa hotelini bila gharama kamili ya malazi kulipiwa kama yalivyokuwa maafikiano katika ziara yake nchini Kenya.

Savage, 38, amelalamika kwamba pia alikosa gari la kumsafirisha kwenda uwanja wa ndege kama ilivyokuwa matarajio.

Anaonekana kugundua kwamba bili ya malazi haikuwa imelipiwa yote wakati wa kuondoka hotelini.


Savage, ambaye jina lake kamili ni Tiwatope Savage-Balogun, alikuwa amezuru Kenya kutumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa almabu mpya ya mwanamuziki nyota kutoka Kenya kwa jina Redsan siku ya Jumamosi. Mwanamuziki wa Jamaica Demarco pia alitumbuiza.

Uzinduzi wa albamu hiyo kwa jina Baddest ulifanyika katika mghahawa maarufu wa Carnivore, na hafla hiyo ilitangazwa sana kwenye mitandao na vyombo vya habari.


Savage amesema alijaribu kumpigia simu promota aliyekuwa amemwalika kuja Kenya bila mafanikio.

Aliwatetea wasanii akisema hawawezi kulaumiwa kwa kulalamika kila mara kuhusu mapromota, iwapo matukio kama hayo yatafanyika.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad