Watu 25,000 Changamoto, Mikopo Elimu ya Juu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watu 25,000 Changamoto, Mikopo Elimu ya Juu
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imebainisha kuwa zaidi ya waombaji wa mikopo ya elimu ya juu 25,000 kwaajili ya mwaka wa masomo 2018/2019, wana changamoto kwenye fomu zao za maombi.


Kupitia taarifa yake HESLB, imefafanua kuwa imepokea jumla ya maombi 78,833 lakini kati yao zaidi ya 25,000 wana makosa mbalimbali ikiwemo kutowasilisha vithibitisho vya sifa ya mtu anayestahili kupata mkopo.

''Baada ya kukamilika kwa muda wa kupokea maombi ya mikopo Julai 31, 2018, HESLB,  imepokea jumla ya maombi 78,833, na baada ya uhakiki, tumebaini waombaji zaidi ya 25,000 fomu zao zina upungufu wa nyaraka na uthibitisho wa kuwezesha kuendelea na hatua inayofuata ya kupangiwa mikopo katikati ya mwezi Oktoba, 2018'' imeeleza taarifa hiyo.

Aidha HESLB imetoa muda wa siku 7 yaani wiki moja kwa waombaji hao kupitia upya fomu zao na kufanya marekebisho kwa njia ya mtandao. Zoezi hilo linaanza leo Jumatatu  Septemba 24 hadi Jumapili  Septemba 30, 2018.

Mbali na hayo bodi ya mikopo pia imewatahadharisha waombaji wa mikopo dhidi ya matapeli wanaolaghai watu kuwa wanaweza kuwasaidia kupata mikopo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad