Wolper Adai Hakuna Msanii Wa Bongo Fleva Anayeweza Kumlipa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wolper Adai Hakuna Msanii Wa Bongo Fleva Anayeweza Kumlipa
Mbunifu wa mavazi na Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi kuwa Video vixen Kwenye video za wasanii wa Bongo fleva.

Wolper ameweka wazi kuwa hawezi kushiriki kwenye video za wasanii wa Bongo fleva kama video queen kwa sababu hakuna mwenye mkwanja mrefu wa kumlipa anachotaka.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Dimba, Wolper amesema kwamba haoni kama kuna msanii anayeweza kuvunja benki kwa kiasi cha pesa anachotaka na badala yake amekuwa akitumia muda wake mwingi kwenye biashara zake.

Ni ngumu kushiriki video ya msanii yeyote kwa sasa. Nina mambo mengi…halafu kiasi cha pesa nitakachohitaji sidhani kama wataweza kunipa”.

Lakini pia Wolper amesema kuwa anashukuru kuona shughuli zake za kumwingizia kipato zinazidi kufanya vyema na kusema ataendelea kuwekeza zaidi kwenye ujasiriamali.

Wolper ameshatokea kwenye video za wanamuziki kadhaa miaka ya nyuma ikiwemo nyimbo ya Diamond Platnumz na Keysha.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad