RC Makonda kuweka kitengo cha uwekezaji kuvutia wawekezaji Dar es Salaam

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

RC Makonda kuweka kitengo cha uwekezaji kuvutia wawekezaji Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ameweka wazi mpango wa kuweka kitengo cha uwekezaji (one stop center) ili kurahisisha uwekezaji na kuondokana na ukiritimba unaosababisha wawekezaji kukata tamaa.

Amesema kitengo hicho kitahusisha watendaji kutoka taasisi za Kituo cha Uwekezaji (TIC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), Idara ya Uhamiaji na wadau wote wanaohusika na biashara na kuongeza kuwa hali hiyo ilikuwa ikisababisha mianya ya rushwa kwa wawekezaji na mwisho wa siku wawekezaji kukata tamaa ya kuwekeza jijini Dar es salaam.

Makonda amesema hayo jijini Dar es Salaam alipotembelea katika Ofisi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na kufanya mazungumzo ya kutafuta namna bora ya kuweka mazingira bora ya kibiashara ili kuondoa kero zinazowakabili wawekezaji na wafanyabiashara jijini humo.

“Naamini ushiriki wa TPSF katika ziara ya Rais Dk. John Magufuli jijini Dar es salaam hivi karibuni, itakuwa fursa kubwa kwa sekta zote ikiwamo biashara, uchumi, afya, elimu, miundombinu na maji hivyo niwahimize watu wote kuitumia vizuri ziara hiyo ili kufikia ndoto ya Dar es salaam kuwa jiji la kibiashara,” amesema Makonda.

Pamoja na mambo mengine, miongoni mwa mambo waliyoridhia kushirikiana ni pamoja na utoaji wa elimu ya biashara, usimamizi wa fedha pamoja na namna bora ya kutumia fursa ya asilimia 10 za mkopo zinazotolewa na serikali kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu ili fedha hizo ziwe na tija.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TPSF, Godfrey Simbeye, amesema taasisi hiyo iko tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mkuu huyo wa mkoa, katika masuala mbalimbali yanayolenga kuliboresha jiji la Dar es salaam.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad