Skendo ya Kubaka Yamnyima Usingizi Ronaldo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Skendo ya Kubaka Yamnyima Usingizi Ronaldo
STAA wa Juven­tus, Cristiano Ron­aldo amedai kuwa kuna watu walifoji taar­ifa zake kuhusu skendo ya ubakaji inayomuan­dama kwa sasa.



Ronaldo ameweka wazi hayo kupitia mwanasheria wake, Peter Christiansen ambaye amedai kuwa kuna nyaraka ziliibiwa na kutu­mika vibaya kwenye skendo hiyo ili kuonyesha ni kweli mteja wake alibaka kitu am­bacho siyo kweli.



Mwanasheria huyo amesema baada ya nyara­ka kadhaa kuibiwa ziliten­genezwa na kubadilishwa ili ionekane Ronaldo alihusika katika kumshawishi mwa­namke aliyefungua kesi kuwa alilipwa ili akae kimya miaka kadhaa ya nyuma.


Kathryn Mayorga akicheza muziki na Cristiano Ron­aldo kwenye uku­mbi wa starehe maeneo ya Las Vegas nchini Marekani

Ronaldo, 33, amekuwa akikana mara kadhaa kuhusika katika kumbaka Kathryn Mayorga wakati walipokutana kwenye uku­mbi wa starehe maeneo ya Las Vegas nchini Marekani mwaka 2009 lakini skendo hiyo imeendelea kumuan­dama na kutishia biashara zake binafsi.



Nyota huyo anadai lengo la skendo hiyo ni kumhar­ibia  sifa na jina lake na hakuna ukwe­li wowote.

I l i d a i w a kuwa mwa­ka 2010, R o n a l d o a l i m p a mw amk e huyo pauni 287,000 ili akae kimya kuhusu skendo hiyo.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad