TFF Wamshangaa Mbeligiji wa Simba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

TFF Wamshangaa Mbeligiji wa Simba
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limemshangaa kocha wa Simba, raia wa Ubelgji Patrick Aussems aliyedai kwamba wachezaji wake wanapewa mazoezi makali ndani ya Taifa Stars ndio maana wanapata majeraha.

Aussems aliwashushia lawama hizo TFF baada ya mchezo wa Simba na Africa Lyon kwa akiwataja zaidi Shomari Kapombe na Jonas Mkude.

Lakini Ofisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema kuwa ni jambo la ajabu hasa kwa mwalimu kusema kuwa mazoezi yanawaumiza wachezaji kwani wanajengwa kwa mazoezi.

“Uwezo wa mchezaji unaongezeka kutokana na mazoezi na kama wao wanalalamika suala hilo basi kuna tatizo hasa kwa wachezaji wenyewe kuwa wavivu kufanya mazoezi ama mazoezi wanayopewa ni rahisi hivyo wamekutana na ugumu ambao umewashtua.

“Timu ipo kwenye maandalizi ya kucheza na Cape Verde hivyo uimara unahitajika ili wachezaji waweze kupambana kiasi kikubwa na kama watafanya mazoezi kidogo jambo hilo halileti afya kwenye soka la ushindani,” alisema Ndimbo.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad