Wasanii wa Bongo Wapeni Haki zao Ma-Producers Kabla Hawajafa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wasanii wakibongo wengi wamekuwa mstari wa mbele sana kulilia haki zao kuwa wanaibiwa (kweli wanaibiwa sana),lakini hivi nyinyi wenyewe hamuoni mnavyowaibia na kuwadhulumu maproducer.Ukienda mbele mtu kama Swizz ,Dr dree mpaka kesho bado wanakula hela ya nyimbo walizo zalisha lkn kwa bongo tofauti maproducer wengi wa zamani wameacha kuzalisha nyimbo.Sio kwamba hawajui au labda wavivu bali music kwao hauwalipi,sababu wanawatajilisha wasanii wao wanakufa masikini.

Wasanii wengi wabongo Fleva wakimwona producer anachipukia wanamkimbilia huyo ili kumlalia ,eti wanaamini kupitia wao wanamtangaza huyo producer,baadaye producer akitaka apate maslahi mapya kwa ajili ya kuboresha maisha yake na studio yake wasanii wengi humkimbia mf tumeiona hii kwa Nareel baada ya kutaka kila ngoma atakayo izalisha basi,lazima awe na mgao wake endapo nyimbo ikitumika kuingiza pesa matakeo yake WEUSI wamekimbia,sasa hivi wapo kwa S2KIZZY.AY na Mwana FA wanaidai Tigo zaidi ya bil 2 ,lkn katika bilioni hizi mbili wamemsahau Harmy B ambaye ndiye aliitengeneza Habari ndio hiyo na wao walimkimbia Harmy B baada yakuweka mikataba ili alinde maslai yake ,Mabeste pamoja na Ve money nao wakamkimbia Harmy B.Hivyo hivyo kwa Macko Chali,Master Jay,P-Funk,Manecky ,Lamar nk hawa wote wametengeneza hit nyingi sana lakini mwisho wa siku wasanii wameishia kuwadhulumu.

Haya Pancho kafa nimemuona ndugu yangu Shetta anasema watz ni wanafiki kisa hawamjali mtu akiwa hai (kweli ndio tabia zetu sisi watanzania), lakini Shetta leo hii nikikuuliza hivi Pancho alingiza Tsh ngapi wakati wewe ukiingiza hela kupitia nyimbo ya Mdananda, Ninauhakika jibu huna zaidi utasema nilimlipa studio session, kumbe hujijui wewe mwenyewe ni bonge la manafiki.

Nikimuuliza Chid Benz moja ya ngoma zake kubwa kuliko zote zisizochuja na ilimpa show nyingi, Je Pancho aliingiza Tsh ngapi ninauhakika jibu litakuwa lile la Shetta, Nikimuuliza Mabeste nae jibu lake litakuwa lile lile

Matokeo yake mnawafanya maproducer wengi waachane na mziki kwani nyinyi wasanii hamuwaheshimu wao ,vipaji vyao pamoja na ubunifu wao wakutengeneza biti ambao unawafanya nini mng'ae.

Sheddy Clever amaproduce hiti tatu za Diamond ambazo zilishika karibia Africa nzima Number One, Nitampata wapi, Marry me (imegonga 6 Platnum=zaidi ya kopi 180000 ), lakini leo nikimuuliza Diamond Je Sheddy alipata Tsh ngapi, jibu litakuwa lile lile kama la Shetta. Abby Daddy nae ameproduce ngoma nyingi za Kiba na moja ya beef lao (inasemekana) baada ya Abby kuweka viwango vipya vya studio na mikataba ya nyimbo anazozalisha, ndugu yangu Kiba akaondoa kwa Abby, lakini nikimuuliza Kiba je Abby alipata Tsh kupitia nyimbo ya Aje, Cheketua nae jibu lake lile lile, eti bila yeye Abby asingekuwa maarufu (upuuzi).

Wasanini mjifunze kuheshimu vipaji na ubunifu wa maproducer wanaowatengenezea beat,kwani bila wao hamna hiti songs,hamna show,wala hela kupitia hizo digital platforms na mjifunze kwathamini pindi wawapo hai kwa kuwapatia haki yao wanayostahili.

Ndio maana leo hii wameibuka maproducer wa hovyo kabisa, wanatengeneza biti zinazofanana ,hamna ubunifu yaani nyimbo siku hizi unasikiliza kwa mazoea wala hushtuki,tofauti kipindi kile cha Majani, Master Jay ,Lamar, Manecky , Mack nk badilikeni mnapodai maslahi yenu mkumbuke kuna maproducer na nyie maproducer jaribuni kujenga umoja wenu ili muweze kutetea maslahi yenu bila hivyo mtaendelea kulalamika na kufa masikini.

By Joseph1989
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad