Watoto Wafanyiwa Upasuaji wa Uti wa Mgongo Wakiwa Tumboni mwa Mama Zao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watoto wafanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo wakiwa tumboni mwa mama zao Watoto wawili ambao bado hawajazaliwa wamefanyika upasuaji wa uti wa mgongo wiki chake kabla ya wao kuzaliwa.

Upasuaji huo ambao ndio ni wa kwanza wa aina yake nchini Uingereza ulifanywa na kundi la madaktari 30 kati chuo kimoja mjini London.

Watoto hao walikuwa na tatizo lilalojulikana kama spina bifida, ambapo uti wa mgongo hukosa kukua vile inavyotakikana na una nafasi ndani yake.

Mara nyingi hali hiyo hutibiwa baada ya mtoto kuzaliwa lakini ikiwa utatibiwa mapema hali ya afya ya mtoto huwa bora.

Wakati wa upasuaji huo uliochukua muda wa dakika 90, madaktari walipasua tumbo la mama kisha wakashona pamoja sehemu ya uti wa mgongo wa mtoto iliyokuwa imeachana.

Upasuaji huo ni hatari sana na unaweza kusababisha mama apatwe na machungu ya mapema ya kujifungua.

Mama wajawazito walihitaji kwenda ng'ambo Marekani, Ubelgiji au Uswizi kufanyiwa uposuaji huo.

"Ni kitu kizuri, alisema Prof David. Wanawake sasa hawahitaji kusafiri kwenda Uingereza. Wanaweza kuwa na familia yao, na gharama ni ya chini. Kwa hivyo mambo yote ni mazuri".

Spina bifida ni nini?
Kulingana na shirika la Charity Shine, zaidi ya watoto 200 huzaliwa na hali hiyo ya spina bifida kila mwaka.

Hali hiyo hutokea wakati kitu kinachoitwa neural tube - awamu ya kwanza ya kukua kwa ubongo na uti wa mgongo hukua kwa njia isiyostahili na husababisha kuwepo nafasi kwenye uti wa mgongo.

Upasuaji unaweza kutumia kuziba nafasi hiyo kwenye uti wa mgongo mara nyingi, lakini mara nyingi matatizo yatakuwa tayari yametokea na miguu kupooza.

Baadhi ya watu hupatwa na hali ngumu ya kujifunza.

Kinachosababisha hali hiyo hakijulikani, ambayo hutokea wakati wa mimba.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad