Ikulu ya Marekani Yamrejeshea Mwandishi wa CNN Kibali ilichofuta

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ikulu ya Marekani Yamrejeshea Mwandishi wa CNN Kibali ilichofuta
Ikulu ya Marekani imerejesha vibali vya mwandishi wa habari wa shirika la CNN chini ya wiki mbili baada ya kufuta vibali hivyo kufuatia majibizano na Rais Donald Trump wakati wa mkutano na waandihi wa habari.

Hii ni siku kadhaa baada ya jaji kuamrisha uongozi wa Trump kumrejeshea mwandishi huyo kibali hicho.

Ikitangaza uamuzi wake, Ikulu ya Marekani pia ilitangaza sheria ambazo zitaongoza mikutano ya baadaye huko White House.

Hii ni pamoja na swali moja kwa kila mwandishi wa habari.

Maswali mengine zaidi yataruhusiwa kwa ruhusa ya rais au afisa ndani ya White House, kwa mujibu wa barua iliyotumwa.

Barua hiyo pia ilionya kuwa hatua zuidi zitachukuliwa dhidi ya Acosta ikiwa hatafuata sheria hizo mpya.

Akizungumzia uamuzi huo wa siku ya Jumatatu wa kurejeshewa vibali vyake, Acosta alisema anataka kurudi tena White House.

Mzozo ulianza kwa njia gani?
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, mfanyakazi wa lkulu alijaribu kuchukua kipasa sauti kutoka kwa Bw Acosta wakati alijaibu kumuuliza Bw Trump maswali zaidi.

Bw Trump alimuita Acosta mtu mbaya na mwandishi huyo akazuiwa kuingia Ikulu siku moja baadaye.

CNN ilipeleka kesi mahakamani kutaka vibali vya Acosta kurejeswa na ikaungwa mkono na vyombo vingine vya habari kikiwemo cha Fox News.

Wakati wa kutolewa uamuzi siku ya Ijumaa jajii mjini Washington alisema uongozi hhaukuwa na sababu za kutosha za kufuta vibali hivyo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad