Msanii Mkono wa Mkonole Aikimbia Ndoa Yake, Aacha Madeni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii Mkono wa Mkonole Aikimbia Ndoa Yake, Aacha Madeni
Aliyekuwa mke halali wa mchekeshaji na muigizaji  Mkono Mkonole ameibuka na kuiambia eNEWZ kwamba mume wake huyo ametoroka nyumbani na kumuachia barua kitandani.


Mke huyo wa Mkono aitwaye Sabrina Ally, amesema baada ya madeni kuwa mengi na kuwazidia yeye na mume wake, ndipo alipoamua kutoroka na kukimbia majukumu huku akiacha barua kitandani ikiwa na maagizo ya kujitosheleza.

Sabrina anasema barua hiyo ilikuwa ina ujumbe ufuatao "Sabrina mke wangu mimi mumeo Fadhili naandika barua hii kwa akili zangu timamu, mimi nimeamua kuondoka kutokana na maisha magumu ambayo tumekuwa tukiyaishi tangu tumeoana nimeamua kuondoka kwenda Kyela kwa mjomba kutafuta maisha na nikipata nitarudi ila sijakuacha mke wangu"aliandika hivyo Mkono.

Sabrina anamalizia kwa kuongea kwamba Mkono alivyoondoka aliacha madeni mengi ikiwepo deni la Benki ambalo liliwekewa dhamana ya hati ya nyumba ya baba yake hivyo pamoja na kwamba Mkono kashaanzisha maisha mengine  anaomba aje alipe deni la watu alilokuwa anadaiwa ili kuzuia nyumba ya baba yake isiuzwe.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad