Wema Sepetu Afikishwa Mahakamani Kesi yake ya Video ya Ngono

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wema Sepetu Afikishwa Mahakamani  Kesi yake ya Video ya Ngono
Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu leo amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili ambapo anashtakiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza video za maudhui ya ngono mitandaoni.

 .

Wema amefika mahakamani hapo majira ya saa 3 asubuhi kiongozana na mama yake mzazi, Mariam Sepetu na wakili wa msanii huyo, Reuben Simwanza, na kwenda moja kwa moja hadi kwenye ukumbi wa mahakama hiyo kusubiri kuanza kusikilizwa kwa kesi yake.

Shauri la kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa katika Maakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya hakimu, Maira Kasonde huku Wakili wa utetezi akiwa Ruben Simwanza na upande wa Jamhuri ukisimamiwa na Wakili Jenifer Masue, lakini imeahirishwa hadi Desemba 12 mwaka huu kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.

Novemba 1, 2018 Wema alipandishwa katika mahakama hiyo akikabiliwa na shtaka la kusambaza video  ya ngono kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, kesi yenye jalada namba KJN/ RB/13607/2018-KUCHAPISHA NA KUSAMBAZA MAUDHUI YA NGONO MTANDAONI.

Wema alisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mahira Kasonde ambapo alikana kosa hilo kisha kuachiwa kwa dhamana ya Shilingi milioni 10 kupitia kwa Salim Limu, ambapo Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 20, mwaka huu (jana) ambapo haikusikilizwa kwa sababu ilikuwa ni Sikukuu ya Maulid.

Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, endapo mtuhumiwa atabainika kusambaza picha au video za ngono au zinazoashiria vitendo vya ngono, adhabu ya kosa hilo ni pamoja na faini ya shilingi milioni 20 au kifungo kisichopungua miaka saba jela au vyote kwa pamoja.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad