Godbless Lema Atuma Ombi kwa Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kuzungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga kwa kile alichodai kuwa ametoa kauli tata.

Lema kupitia ukurasa wake wa kijamii leo, Disemba 16, ameandika kuwa kauli ya Gavana ambayo hakuianisha ni kauli ipi, kuwa endapo isipoeleweka hata kama iliongelewa kwa nia njema itakuwa ni hatari kwa mstakabali wa uchumi.


"Mh Rais tafadhali kwa heshima kabisa ongea na Gavana wa Benki kuu ,kwa maoni yangu Gavana anaongea sana.Kauli ya Gavana hata kama ina nia njema ikishindwa kueleweka mara nyingi huwa ni hatari kwa uchumi na uimara wa shilingi. Sina uhakika kama utadumu naye muda mrefu kazini", ameandika Lema.



Novemba 20, katika mkutano wake  na wanahabari, Prof. Luoga alisema kuwa taasisi hiyo imeanzisha operesheni maalum ya ukaguzi na udhibiti wa uendeshaji biashara ya fedha jijini Arusha, ikiwa ni siku moja tangu kutokea sintofahamu katika biashara ya maduka ya kubadilishia fedha jijini humo baada ya kufungwa kwa saa kadhaa.

“Uchunguzi wa Benki Kuu umebaini kuongezeka biashara ya ubadilishaji na utakatishaji fedha. Kuna maduka hayajasajiliwa lakini yanafanya biashara hii kinyume cha utaratibu,” alisema Profesa Luoga.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad