Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania AKANUSHA Tuhuma za Fastjet Kuzuiwa Kuingiza Ndege Nchini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania AKANUSHA Tuhuma za Fastjet Kuzuiwa Kuingiza Ndege Nchini
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Hamza S. Johari  leo Disemba 27, 2018 amezungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Kampuni ya Fastjet  kuzuiwa kuingiza ndege hapa nchini pamoja na tuhuma kibao walizozitoa wakidai AirTanzania inapendelewa.

1.FastJet hawakuwa na ndege hata moja hivyo kama mamlaka ya TCAA hatuna budi kuwazuia, wanamadeni ya 6 billion  japo wamelipa kidogo, lakini sheria inawataka walipe yote, hivyo kama wao wanahitaji kufanya biashara wafuate masharti na walipe madeni.

2.Tulipata taarifa kupitia vyombo vya habari kwamba tarehe 22 Disemba 2018  wangeleta hizo ndege zao, lakini mamlaka haikuwa na taarifa hizo na wao utaratibu wa kuingiza ndege nchini wanaujua.

3.Ilipofika Tarehe 24 Disemba 2018  saa 6 mchana ndo wakatuma email  ya maombi ya kuleta ndege  hizo zenye usajili wa Afrika Kusin.

4.Ikumbukwe kwamba, tarehe 25 ilikuwa ni sikukuu na tarehe 26 ilikuwa ni Boxing Day hivyo sote hatukuwa ofisini. Wanaposema et tumewazuia kuzileta ni waongo.

5.Katika notisi ya siku 28 tuliyowapa, tuliwataka Fastjet walete andiko la kudhibitisha uwezo wa kufedha ili kuona kama wanajiweza na pia walete Meneja Mwajibikaji mwenye utaalamu na mambo ya ndege. Fastjet hawakuletea hivyo vitu

6.Badala yake Tar 24.12.2018  ndo sasa wakaleta  maombi na barua ya mkurugenzi mtendaji wa Fastjet  Lawrence Masha  wakitujulisha kuwa Lawarence Masha amejiteua mwenyewe  kuwa accountable manager.

7.Fastjet waache mzaha. FastJet itakufa kwasababu zao wenyewe maana wanamatatizo mengi, TCAA tunasimamia sheria ili kulinda usalama wa abiria, kulinda maslahi ya watoa huduma (supplies). Habari zote zilizoelezwa si za kweli ni upotishaji mtupu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad